kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini?
Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.
Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa
waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini
angalau wanaupata kwa kiwango fulani. Wakati waganga hawa wanawasaidia watu
kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi. Sasa kwa
nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina
maana wao hawapendi utajiri huo?
Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri.
Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio
yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. Na watu hawa huambiwa
wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya
ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa
juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. Kwa mfano mganga
anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani
ndio aende kwenye biashara zake. Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na
mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye
mafanikio yake.
Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama
kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha
atafilisika.
Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa
hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia
mafanikio makubwa. Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe,
kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata
muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.
Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu
aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani
anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio. Ili
kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo
litamuondolea woga kabisa. Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba
ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.
Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu
ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo
kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la
kuweza kufikia mafanikio.
Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.
Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa
kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.
Kwa nini watu baadae hufilisika?
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio
wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa
kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe.
Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.
Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi.(Mwezi
huu kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunajifunza jinsi ya kujijengea nidhamu binafsi,
karibu ujifunze). Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na
hakikisha unayafuata.
Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka
saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. Baada ya hapo
unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia
unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye
kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.
Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa
kwenye maisha yako na shughuli zako.
Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia
mafanikio;
1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na
imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.(tulijifunza wiki
iliyopita)
2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals)
na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku(routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe
na vifuate kila siku kwenye maisha yako.
Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia
mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka
unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda
kwa mganga, uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.
Thanx bro nimekuelewa sijui nakupata vp private kuhusu saikoloji
ReplyDelete