YAWEZEKANA
! Unasoma sana lakini matokeo yakitoka hutamani rafiki au hata wazazi wako
wajue kile ulichopata AU unafanya vizuri darasani na mitihani ya kawaida lakini
inapofika muda wa kufanya mitihani ya mwisho kama vile ya END OF SEMISTER
unafeli mpaka unahisi unafanyiwa hila au umelogwa!. Kufeli sio jambo zuri kwa
mtu kulipata katika kitu chochote hasa ukiwa shuleni,kwa kutambua hilo
haijalishi wewe ni mwanafunzi wa shule ya hadhi gani au unarudia mtihani au
wewe ni WA UELEWA GANI huna budi kujua njia hizi rahisi sana za kukusaidia kufaulu
mitihani yako.
1 . SOMA MITIHANI ILIYOPITA. (past papers)
Njia hii ni rahisi sana itakusaidia sana kujua namna ya kujibu maswali,kujua
mitego na mbinu za watunga mitihani ambao mara nyingi hurudia maswali yaleyale
kwa namna tofauti, vilevile itakusaidia kujua format au miundo ya mitihani na
hii itapelekea wewe kujua majibu ya maswali mengi sana ndani ya muda mfupi
sana.Mbinu hii itakusaidia sana kufaulu mitihani.
2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOLISOMA. (Topics)
Kujua topic za kila somo unalotarajia kujibu mtihani wake kutakusaidia sana
kujua mada zipi huwa na maswali mengi,alama nyingi,mada zenye maswali rahisi na
magumu.Hii inakupa mwongozo sahihi sana wa kujua wapi pa kuanzia pindi
unavyojiaandaa kujibu mtihani.Ni hatari sana kuingia kwenye chumba cha mtihani
ukiwa hujui maswali yapi ya kuanza kwenye mtihani husika hata kama unajua vitu
vingi vya kujibu.Hivyo kujua topic ni njia rahisi sana kuelekea kufaulu mtihani
wako.
3. SOMA KWA LENGO. (Target)
Kusoma sio hekali za shamba unazotakiwa kutumia muda mrefu sana ili umalize
kuzilima la hasha ! kusoma ni kazi inayohusisha akili na viungo hivyo unatakiwa
kuwa na lengo maalumu kila unaposoma sio kusoma ilimradi.Ni heri ulale
upumzishe akili kuliko kusoma ukiwa hauelewi kitu husika unachokisoma kina
faida gani kwako.Ndio maana wapo baadhi ya wanafunzi wanaotumia muda mrefu
hufeli wakati wapo watu wanaofaulu licha ya kutoingia darasani wala kusoma muda
mrefu .Hii ni kwa sababu wengi wa wanafunzi wanaosoma muda mrefu husoma bila ya
kujua lengo la kusoma vitu au mada fulani na kuishia kufeli.Hivyo kujua unasoma
kitu fulani kwa ajiri gani kutakupa uhakika mkubwa wa kufaulu amini.
4. TUMIA MUDA MWINGI KUSOMA MASOMO UNAYOYAELEWA VIZURI. (uwekejazi)
Usielewe vibaya ! Kutumia muda mwingi kwenye masomo unayoyaelewa vizuri
haimanishi uache kusoma masomo mengine,ila hii ina maana kwamba unatakiwa
kuelewa zaidi na zaidi na kugeuza masomo yote unayoyaelewa kama uwanja wa
nyumbani kiasi kwamba katika mitihani ya masomo hayo unakuwa na uhakika wa
kupata zaidi ya 65% mpaka 75% . Mbinu hii ni rahisi sana na muhimu maana ufaulu
hutegemea alama za masomo tofauti tofauti na sio somo moja tu.Hivyo jua zaidi
kwenye masomo unayoyaelewa yatakulipa kwenye mitihani na kukupa uhakika wa
kufaulu.
5. SOMA NOTES FUPI ZENYE KUBEBA MAWAZO YA MSINGI. (kupunguzia kichwa mzigo)
Badala ya kusoma maelezo mengi kama msomaji wa risala , Notes fupi zilizo
andaliwa vizuri zitakusaidia kufaulu mtihani kirahisi.Njia hii itakusaidia
kutokuishiwa hamu ya kusoma unapotumia notes fupi,husaidia kuelewa haraka na
kwa mujibu wa wataalamu wanadai Notes fupi husaidia sana kumtunzia mwanafunzi
kumbumbu nzuri.Hivyo tumia notes fupi, mfano mzuri wa notes fupi na nzuri ni
zile zinazotolewa na application ya “thl tanzania” kwenye vifaa vya elektroniki
simu,tablets n.k , vitini ,vitabu na vipeperushi mbalimbali.” Zingatia”(
Hakikisha notes zako fupi zinaendana na kile ambacho mtaala unachohitaji
ukisome vilevile Njia hii inaweza kutofanya vizuri sana kwenye baadhi ya masomo
mfano hisabati;fizikia na kemia na biologia,hivyo kwa masomo haya notes fupi
lazima zipewe uungwaji mkono na mazoezi ya mara kwa mara japo kwa baadhi ya
watu sio lazima).
6. BUNI KANUNI ZA MAJIBU. (kuwa mbunifu)
Kubuni Kanuni ni ujanja wa aina yake asikudanganye mtu.Elewa kwanza hizi sio
kanuni rasmi bali ni kanuni ambazo mtu anabuni kwa namna yake akiwa na lengo
zimsaidie kutunza kumbukumbu na zimrahisishie anapojibu maswali.Yawezekana
hujaelewa vizuri bado usijali ,,, Mfano mzuri wa kanuni za kubuni ni ule watoto
wa shule ya msingi hufundishwa ili kukariri haraka vipimo vya urefu yaani;”
Kofia Huuzwa Dukani Mwa Daudi Senti Mia” ikimanisha Kilomita, hektomita,
dekamita, Mita,Desimita,Sentimita na Milimita. Hivyo ukitulia kwa kila somo
lolote unaweza kubuni kanuni hizi ambazo zitakurahisishia sana kujibu maswali
na kukupa uhakika wa kufaulu.
7.FANYA TATHMINI NA FAHAMU MUDA ULIOSALIA KABLA KUFANYA MTIHANI. (uandaaji wa
silaha)
Hii ni njia rahisi sana inayoweza kukufanya ufaulu mtihani tena ukiwa na
uhakika.Tathimini ndio kipimo sahihi kitakacho kufanya ujue upungufu wako uko
wapi na nini ufanye kulingana na muda ambao utakuwa umesalia kabla ya kufanya
mtihani. Zingatia “tathimini” hii unatakiwa uifanye ukiwa peke yako au na mtu
mwenye kukutakia mema kama vile rafiki yako unayesoma naye ,hapo mtagundua wapi
panawasumbua na kujua wapi pakupata msaada kabla ya mtihani.Mitihani ya
kujiandaa haitoshi kukwambia uko sawa ila inahitaji wewe ufanye tathimini
sahihi ujue unachotakiwa kufanya kabla ya mtihani.
8. KUTANA NA WENZAKO KABLA YA SIKU AU MASAA MACHACHE KABLA YA MTIHANI
.(discussion yenye mafanikio)
Hapa elewa kwanza kwenye suala la discussion kuna watu aina mbili darasani au
katika kusoma;wapo watu wanopenda sana discussion lakini lazima tuelewe kuwa
kuna watu wengine hawapendi kabisa kusikia kitu kama hicho sio kwamba hawapendi
ushirikiano na wenzake bali hujisikia huru sana wakiwa wanasoma peke yao.Ikiwa
wewe ni miongoni mwa watu wa kundu hili hapa panakuhusu .Raha ya kusoma ni
kufaulu hivyo kuna hamu kubwa ya kusoma siku chache kabla ya mtihani .hivyo
kama wewe hupendi discussion za kila siku discussion kabla ya kufanya mtihani
zitakusaidia sana kujua mbinu za wenzio ukichanganya na zako utapata
kitu.chukueni na fanyeni past papers pamoja,utapata pointi nyingi sana na
haitakuwa rahisi wewe kujisahau kama unajiamini kwenye kutunza kumbukumbu
nakujibu mtihani kirahisi.
9. ELEWA MAZINGIRA NA HISTORIA YA MITIHANI. (kuwa mtabiri)
“ Ni rahisi sana kupata O% kwenye mtihani wa TESTS lakini sio rahisi kupata
O% kwenye mtihani wa END OF SEMISTER” .Watu hawalielewi hili ,ASSIGNMENTS NA TEST siku zote Huzingatia kupima wanafunzi wa kila aina .Hivyo maswali hutolewa kwa kuzingatia kwa kile mlichosoma tu hata kama kidogo kiasi gan lakin END mtihan hupitiwa na wakubwa kuhakikisha umezingatia topics zote zilizopangwa kufundishwa kwa semister
10.TULIA,KUWA NA AMANI FANYA MTIHANI.( usiwaze kuhusu matokeo,likizo au
kumaliza shule)
TULIA !!! Unawaza kuhusu kumaliza mtihani sio?! Tulia ratiba ikiisha utarudi
mtaani, hivyo usiruhusu kufikiria mambo mengine badala ya mtihani muda wa
mtihani, japo hutokea kwa baadhi ya watu .mfano wale wanaofikwa na matatizo
mbalimbali kabla au kipindi cha mtihani sio rahisi kutofikiria matatizo
hayo,lakini usijali….Jitahidi kuwa Strong na muombe MUNGU.Lakini kama hauna
tatizo lolote muda wa mtihani sio muda wa kufikiria kuhusu likizo au nini
utafanya baada ya mtihani ,muda wa mtihani ni muda wa kuandaa kile kitakacho
onekana baada ya mtihani na si vinginevyo.Ingawa wapo watu wengi sana wanaotumia
muda huu vibaya kwa kuwaza nyumbani,na mambo mengine yasiyo sahihi kwa muda
huo. Tasisi za Elimu au shule si miaka ya kukufanye ukue bali ni mahali ambapo
wazazi,walezi au hata taifa linategemea utoke na ujuzi utakotufaa watu wote
hivyo tafadhali usituangushe.
ZINGATIA:
Njia hizi ni za uhakika kutokana na mafanikio watu wengi waliotumia njia hizi
kufaulu.Kila mtu ni shahidi mazingira ya shule nyingi si rafiki sana kwenye
kufaulu kutokana na mapungufu mbalimbali ambayo serikali haiwezi kuyatatua peke
yake.hivyo hakuna wa kumlaumu kwenye matokeo mabovu yanayotokea maana serikali
ni Mimi,wewe na yule tushirikiane,watu wafaulu nchi iwe na wasomi wenye kuelewa
mambo .LAKINI tusiishie kufaulu bila ya kuwa wabunifu maana hakuna tutakacho
kuwa tunakifanya.SOMA, FAULU, KUWA, MBUNIFU TUPATE MATOKEO MAZURI
NA EVANCE CONDRAD SOMBE
0762239504
KWA HABARI ZAIDI ANDIKA EMAIL YAKO NA SUBMIT ILI UWE UNAPATA HABARI ZOTE KILA ZINAPOTOKEA. JUU UPANDE WA KULIA
No comments:
Post a Comment