Katika Kanisa Katoliki linatumika hasa[1] kwa waumini wafu ambao maisha yao yameanza kuchunguzwa ili kuona kama hatimaye wataweza kutangazwa watakatifu
.
HATUA YA KUITWA MTUMISHI WA MUNGU[
2][3]
Jina Mtumishi wa Mungu halimaanishi kuwa kweli mhusika alimtumikia Mungu kiaminifu hadi kifo chake, bali kwamba watu wengiwengi wanaona hivyo, hata askofu wa jimbo alifungua kesi ya kumtangaza mtakatifu.
Baada ya hatua hiyo kukamilika kwa Papa kuthibitisha ushujaa wa maadili yake yote, au kifodini chake, mtumishi huyo ataanza kuitwa Mstahili heshima.
Kisha kuthibitisha kwamba muujiza wowote umetokea kwa maombezi yake, Papa atamtangaza mwenye heri.
Baada ya muujiza mwingine atamalizia kwa kumtangaza mtakatifu.[4][5]
Kesi hizo katika hatua zote zinasimamiwa na idara maalumu yenye makao makuu huko Vatikani.
Tofauti na hilo ni jina Servus Servorum Dei (Mtumishi wa mtumishi wa Mungu), ambalo kuanzia Papa Gregori I linatumiwa na Mapapa kujitambulisha.
MSTAHILI HESHIMA
Uchunguzi huo unahusu maadili ya Kimungu (imani, tumaini na upendo), maadili bawaba (busara, haki, nguvu na kiasi) pamoja na unyenyekevu. Kwa watawa unachunguzwa pia utekelezaji wa nadhiri zao.
Pamoja na hayo, Kanisa linasubiri Mungu athibitishe mwenyewe kwa muujiza mmoja iliyopatikana kwa maombezi ya huyo ili aweze kutangazwa mwenye heri na wa pili ili atangazwe mtakatifu.
MWENYE HERI
Mwenye heri ni jina la heshima analopewa Mkristo wa Kanisa Katoliki baada ya kufa na ya kufanyiwa kesi makini kuhusu ushujaa wa maadili yake yote na juu ya muujiza mmoja uliofanywa na Mungu kwa maombezi yake baada ya kifo chake.
Kwa mfiadini inatosha kushuhudia kwa hakika kwamba aliuawa kwa ajili ya imani au adili lingine.
Asili ya hatua hiyo ni karne XIV ambapo Papa alianza kukubali marehemu aheshimiwe kwa namna ya pekee mahali fulani au katika shirika fulani kabla kesi ya kumtangaza mtakatifu kwa Kanisa lote haijakamilika
HATUA YA KUITWA MTAKATIFU
Kwa Wakatoliki mtakatifu ni yule aliyemfuata Yesu Kristo, akiishi kwa upendo na maadili mengine yanayoutegemea, hasa aliyeyatekeleza kwa kiwango cha ushujaa katika kufia dini au katika maisha ya kila siku.
Utakatifu si wa aina moja, bali kila binadamu anatakiwa kuitikia siku kwa siku wito maalumu aliopewa na Mungu. Hivyo yeyote anaweza na kupaswa kulenga utakatifu, bila kujali sifa zake za kibinadamu tu.
Ili kuzuia udanganyifu, Kanisa Katoliki linamuachia Papa kusimamia kesi ndefu za kumtangaza mtakatifu mpya, miaka baada ya kifo chake.
Wakatoliki wanawapatia Bikira Maria na watakatifu wengine heshima ya pekee kama marafiki wa Mungu, lakini si ibada halisi. Heshima hiyo inadai wajitahidi pia kufuata mifano yao kama wao walivyofuata ile ya Yesu
NA EVANCE SOMBE
0762239504
No comments:
Post a Comment